Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2017
Picha
Msanii wa maigizo aliyefanya vizuri na filamu ya 'Mapenzi ya Mungu', Elizabeth Michael ' Lulu' amefunguka na kusema wasanii wa maigizo bongo wanafeli kutokana na kutojielewa ni kitu gani ambacho wanakitaka kwenye sanaa, badala yake wanafuata mikumbo. Lulu amefunguka hayo hivi karibuni akizungumza na wanahabari na kusema kuwa wasanii wengi wa Tanzania hawapendi kujishughulisha kutafuta kitu kizuri kwa kuwa wengi wao walifuata mkumbo kwenye kuigiza na wengine walichukulia kama sehemu ya kujipatia umaarufu ili maisha yaendelee au sehemu ya kupotezea muda. "Ukweli upo kwenye uigizaji kuna watu tunachukulia hii ni kazi, wapo wanaofanya kama sehemu ya kipaji chake lakini pia wapo ambao wanachukulia kama sehemu ya kujipatia umaarufu au ku-refresh kwani wanakua na kazi zao zingine, na hao ndio wanaosababisha tuonekane waigizaji wa muvi tumefeli". Pamoja na hayo Lulu ameongeza, "Unajua pia kufuata mkumbo ni kitu kilichoturudisha nyuma. Watu wengi walikuwa wa