MAREKANI YATISHIA VIKWAZO KWA YEYOTE ATAKAEKWAMISHA UCHAGUZI DRC

Marekani yatishia vikwazo kwa yeyote atakaekwamisha uchaguzi DRC Serikali ya Marekani juma hili imetishia kuwawekea vikwazo wale wote watakaobainika wanakwamisha kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC. Kauli ya Marekani imekuja wakati huu mwishoni mwa juma lililopita mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo, CENI Corneil Nangaa alitangaza kuwa tume yake haiwezi kuandaa uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu. Kuendelea kucheleweshwa kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa DRC huenda kukasababisha kuzuka kwa machafuko zaidi nchini humo ambapo katika maandamano ya mwaka jana mamia ya watu walipoteza maisha. Naibu balozi wa Marekani kwenye baraza la usalama la umoja wa Mataifa, Michele Sison amesema kuwa nchi yake iko tayari kutangaza vikwazo dhidi ya mtu au kundi la watu watakaobainika wanakwamisha kufanyika kwa uchaguzi huru na wa kidemokrasia. Nchi ya Marekani mwaka jana ilitangaza vikwazo kwa maofisa kadhaa wa juu wa Serikali ya DRC ikiwa ni pamoja na kuzuia mali na fedha zao na kuzuia raia wake kufanya biashara za watu waliowekewa vikwazo. Hayo yakijiri shirika lisilokuwa la kiserikali linalotetea haki za binadamu la ACAJ nchini Jamhuri ya kimokrasia ya Congo limetoa wito wa kuachwa huru mara moja kwa wanaharakati wawili ambao walionyesha kupinga kauli ya tume huru ya uchaguzi CENI kuwa haiwezekani uchaguzi ufanyike mwaka huu wa 
2017 nchini humo. Na beka

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UTAMBURISHO WA DANI ALVES PSG

Sanjay Dutt kuifaidi Tanzania siku 21