Machapisho

Tunatafuta u star ili tupate pesa ISMAYA KIDUKU

Picha
T unautafuta u star sio kwasababu ya mademu tunautafuta u star kwa sababu ya kutengeneza pesa na kama unaona kuna vijana wanataka kuwa ma star ili wapate watoto wazuri basi mi naona hawana akili timamu na awawezi kufika mbali watapotea mimi binafsi nataka kufanya umaarufu wangu kuwa mtaji wa kuniingizia pesa hivyo yani.  alijibu ismaya kiduku baada ya kuulizwa swali la kizushi kuhusu kutafuta u star kwake ISMAYA KIDUKU
Picha
Msanii wa maigizo aliyefanya vizuri na filamu ya 'Mapenzi ya Mungu', Elizabeth Michael ' Lulu' amefunguka na kusema wasanii wa maigizo bongo wanafeli kutokana na kutojielewa ni kitu gani ambacho wanakitaka kwenye sanaa, badala yake wanafuata mikumbo. Lulu amefunguka hayo hivi karibuni akizungumza na wanahabari na kusema kuwa wasanii wengi wa Tanzania hawapendi kujishughulisha kutafuta kitu kizuri kwa kuwa wengi wao walifuata mkumbo kwenye kuigiza na wengine walichukulia kama sehemu ya kujipatia umaarufu ili maisha yaendelee au sehemu ya kupotezea muda. "Ukweli upo kwenye uigizaji kuna watu tunachukulia hii ni kazi, wapo wanaofanya kama sehemu ya kipaji chake lakini pia wapo ambao wanachukulia kama sehemu ya kujipatia umaarufu au ku-refresh kwani wanakua na kazi zao zingine, na hao ndio wanaosababisha tuonekane waigizaji wa muvi tumefeli". Pamoja na hayo Lulu ameongeza, "Unajua pia kufuata mkumbo ni kitu kilichoturudisha nyuma. Watu wengi walikuwa wa
Picha
PICHA : Mazishi ya Mke wa Waziri Mwakyembe leo Mbeya By lilian July 19, 2017 SHARE TWEET SHARE SHARE COMMENTS Mamia ya Wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama na dini wameungana na familia katika mazishi ya aliyekuwa mke wa Waziri wa Habari Dr. Harrison Mwakyembe, Linah George Mwakyembe yaliyofanyika leo July 19, 2017 Mbeya. SHARE

Sanjay Dutt kuifaidi Tanzania siku 21

Picha
MUigizaji mkongwe na  anayefanya vizuri kwenye soko la filamu India, Sanjay Balraj Dutt, aliyekuja nchini kwa ajili ya mapumziko anatarajiwa kudumu kwa siku 21 ambapo atatembelea mbuga za wanyama na vivutio mbali mbali vilivyopo nchini. Muigizaji Sanjay Balraj Dutt. Ujio wa Sanjay Dutt umethibitishwa na mwenyeji wake ambaye ni Mbunge wa Manonga, Seif Gulamali ambaye amesema uwepo wa msanii huyo ni kipimo cha kuwa sekta ya utalii nchini inaendelea kupanuka. "Uwepo wa Sanjay Dutt nchini ni fursa kubwa sana. Wahusika wa utalii hapa nchini wakiona fursa katika kuutangaza zaidi utalii wetu ni vyema pia wakamtumia kwani mtu huyu ni mkubwa sana kwenye sanaa ya filamu. Lakini pia kuja kwake hapa nchini ni wazi tunazidi kukua kwenye sekta hii, na tutapata mapato kupitia kuwepo kwake kwani atakuwepo kwa takribani siku 21" alisema Mhe. Gulamali Muigizaji Sanjay Dutt (kushoto) akipeana mkono na Mbunge Gulamali Hata hivyo mbunge huyo amewat

CHIDBENZI AMCHANA ZILLA

Picha
FATUMA MUNA Rapa Chid Benz amemtaka Rapa Godzillah kupunguza maneno yasiyo ya msingi kwenye nyimbo zake na badala yake afanye muziki mwepesi utakao burudisha watu na siyo kuandika kizungu kingi kinachompotezea mashabiki. Chid amesema kwamba Godzillah alikuwa muandishi mzuri wakati anaingia kwenye game lakini kwa sasa amekuwa muandishi anayeandika vitu vingi kupitiliza kitu ambacho kinamfanya aonekane kama mtu asiyejua anataka nini kwenye uandishi wake. "Godzilla ni muandishi mzuri sana, nyimbo zake alikuwa anajua kipi aandike kipi aache lakini siku hizi amekuwa anaandika kupita kiasi hadi kuonekana kama mtu aliyechanganyikiwa. Namshauri mdogo wangu afanye muziki mwepesi ambao kama ule alioanza nao kwani alijipatia mashabiki wengi. Pia aachane na hayo makundi ya watu wanaoimba kingereza halafu lugha yenyewe hawaijui hii inamuharibia sana",  amesema Chid Benz Vile vile Chid ameongeza kwamba  "Godzilla sasa hivi nyimbo zake za zi

UTAMBURISHO WA DANI ALVES PSG

Picha
Dani Alves amesema hajutii kusajiliwa na Paris Saint-Germain,Walimpa ofa ya mshahara wa Pound 230,000 kwa wiki,Anasema amekuja Ufaransa kuwa Mshindi. Dani Alves alitambulishwa rasmi kama mchezaji wa PSG kutoka Juventus jijini Paris wiki hii na mke wake mwanamitindo Joana Sanz alikuwepo. Dani Alves pia alitoa ujumbe kwa kocha wa Manchester City,ep Guardiola nakusema Samahani kwa kuamua kujiunga na PSG, nimekuja Ufaransa kuwa mchindi. Dani Alves akiwa PSG kwa mwaka atatengeneza pound milioni 12.

MAREKANI YATISHIA VIKWAZO KWA YEYOTE ATAKAEKWAMISHA UCHAGUZI DRC

Picha
Marekani yatishia vikwazo kwa yeyote atakaekwamisha uchaguzi DRC Serikali ya Marekani juma hili imetishia kuwawekea vikwazo wale wote watakaobainika wanakwamisha kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC. Kauli ya Marekani imekuja wakati huu mwishoni mwa juma lililopita mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo, CENI Corneil Nangaa alitangaza kuwa tume yake haiwezi kuandaa uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu. Kuendelea kucheleweshwa kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa DRC huenda kukasababisha kuzuka kwa machafuko zaidi nchini humo ambapo katika maandamano ya mwaka jana mamia ya watu walipoteza maisha. Naibu balozi wa Marekani kwenye baraza la usalama la umoja wa Mataifa, Michele Sison amesema kuwa nchi yake iko tayari kutangaza vikwazo dhidi ya mtu au kundi la watu watakaobainika wanakwamisha kufanyika kwa uchaguzi huru na wa kidemokrasia. Nchi ya Marekani mwaka jana ilitangaza vikwazo kwa maofisa kadhaa wa juu wa Serikali ya DRC ikiwa ni pamoja na kuzuia m